JE KAMA UKIUTAFUTA KWANZA UFALME WA MUNGU UTAPATA NINI?

Hello habari ndugu? Karibu tena siku ya Leo tena tunapoendelea kujifunza zaidi kuhusu neno la Mungu pamoja na mbinu mbalimbali za mafanikio, ujasiriamali na biashara. Leo nitazungumzia suala la maisha yetu ya kawaida kabisa. Watu wengi tumekuwa tukihangaikia maisha ambalo ni jambo zuri sana kwa sababu ndipo tunapopapata ridhiki yetu ya kila Siku. Lakini leo ndugu nataka turudi kwenye maandiko matakatifu yaani biblia kuhusu suala la utafutaji na je inatuhasa tutafute kitu gani kwanza ili tuweze kupata mafanikio Yetu ya kimwili Na kiroho pia. Naomba usome na mimi kwenye biblia katika kitabu cha MATHAYO 6:33-34 kama ifuatavyo; 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Kwa hiyo rafiki yangu nakushauri sana jitahidi kutafuta ufalme wa Mungu kwanza kabla ya kitu chochote hapa duniani na hapo ndipo Mungu atakubariki hata kazi ya mikono yako. Una...