JE NI SAUMU IPI INAKUBALIKA MBELE ZA MUNGU?

JE UMESHAWAHI  KUJIULIZA NI KWA NINI TUNAFUNGA NA KUOMBA?

NA JE NI SAUMU IPI INAYOKUBALIKA MBELE ZA MUNGU?

WATU WENGI TUMEKUWA TUKIFUNGA NA KUOMBA LAKINI HATUPATI MAJIBU YA MAOMBI  YETU KAMA WALIVYOKUWA WANA WA ISRAELI KATIKA KITABU CHA ISAYA 58:3-5

LAKINI UKISOMA KATIKA ISAYA 58:6-7 INAELEZA MAMBO 8 YA KUZINGATIA ILI SAUMU YETU IKUBALIKE MBELE ZA MUNGU NAYO NI

1. KUFUNGUA VIFUNGO VYA UOVU

2. KUZILEGEZA KAMBA ZA NIRA.

3. KUWAACHIA  HURU WALIONEA

4. KUVUNJA KILA NIRA.

5. KUWAGAWIA WENYE NJAA CHAKULA CHAKO.

6. KUWALETA MASKINI WALIOTUPWA NJE NYUMBANI KWAKO.

7. UMWONAPO  MTU ALIYE UCHI, UMVIKE NGUO

8. WALA USIJIFICHE NA MTU MWENYE DAMU MOJA NAWE.

BASI  NDUGU TUZINGATIE MAMBO HAYA ILI MAOMBI NA SAUMU ZETU IKUBALIKE  MBELE ZA BWANA.

Wako katika ujenzi wa Taifa
Mwalimu Caleb Samuel Bandora.

BONYEZA MAANDISHI HAYA ILI UJIUNGE NAMI NIWE NAKUTUMIA MAKALA NZURI NA MASOMO YA NENO LA MUNGU , UJASIRIAMALI, BIASHARA NA MAFANIKIO KWA NJIA YA EMAIL KILA WIKI


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FURAHA YA BWANA NDIYO NGUVU YANGU

MADHARA UTAKAYOPATA KAMA USIPOTUMIA KIPAJI CHAKO