MADHARA UTAKAYOPATA KAMA USIPOTUMIA KIPAJI CHAKO

Leo napenda nizungumze na wewe rafiki yangu juu ya talanta au kipaji chako ulichopewa na Mungu . Yawezekana rafiki yangu wewe una kipaji cha uimbaji au uchoraji  au uandishi au uigizaji  n.k.  Pia labda wewe umepewa kipaji au Huduma Fulani ambayo unatakiwa kumtumikia Mungu kupitia hicho kipaji au Huduma uliyopewa Mungu. Lakini yawezekana haujatumia kipaji au talanta kutokana sababu au visingizio mbali mbali kama kutokujiamini , kujisikia , maringo, ulegevu, uvivu au unataka hadi ubembelezwe na sababu zingine kadhalika


Naomba usome biblia  na mimi katika kitabu cha MATHAYO 25: 14-30. Hii imelezea watumishi watatu walioachiwa talanta na bwana wao. Mmoja alipewa talanta kumi, mwingine  talanta tano na mwingine talanta moja. Aliyepewa talanta kumi alienda akafanya biashara akapata talanta kumi nyingine vivyo hivyo aliyepewa talanta tano akazalisha talanta tano zingine baada ya kufanya biashara. Lakini aliyepewa talanta moja akachimba shimo akaifukia talanta yake akiogopa isije ikapotea. Lakini yule tajiri aliporudi akauliza hesabu ya mali alizowapa ndipo akawapongeza sana wale watumishi wake wawili waliozalisha na kupata faida ya mali alizowapa kama mtaji kisha akawapatia zawadi. Lakini yule mtumishi mpumbavu akamwambia tajiri yake kwamba tajiri yake ni mtu mgumu tena anavuna asipopanda na ndio mana akaamua kufukia  talanta yake aliyopewa. Ndipo yule tajiri akaamua yule Mtumishi mpumbavu anyan'ganywe talanta yake hiyo moja  kisha akapewa mwingine  kisha akamfukuza


Hii hadithi inatupa FUNZO KUBWA sana juu ya talanta au vipaji tulivyopewa na Mungu kwamba baada ya kutumia talanta lazima tutatoa hesabu ya uzalishaji Na matokeo ya matumizi ya vipaji vyetu kama tulileta faida au hasara kwenye jamii yetu. Kwa hiyo ndugu yangu usipotumia kipaji chako utanyan'gwanywa na atapewa mwingine anayefanya vizuri zaidi yako.


USHAURI WANGU BINAFSI KWAKO rafiki yangu kama haujaanza kutumia talanta au kipaji ulichopewa anza kukitumia sasa jifunze na jiongezee maarifa zaidi ni jinsi gani utaanza kutumia kipaji chako ili uisadie jamii yako iliyokuzunguka (USIFUKIE TALANTA AU KIPAJI CHAKO KAMA  YULE MTUMISHI MPUMBAVU) au kama unakitumia vibaya katika namna ambayo haimpendezi Mungu ACHA !

Wako katika ujenzi wa Taifa
Mwandishi : Mwalimu Caleb Samuel Bandora

BONYEZA HAYA MAANDISHI ILI UJIUNGE NAMI NIWE NAKUTUMIA MAKALA NZURI NA MASOMO YA NENO YA NENO LA MUNGU, UJASIRIAMALI, BIASHARA NA MAFANIKIO KWA NJIA YA EMAIL KILA WIKI



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FURAHA YA BWANA NDIYO NGUVU YANGU

JE NI SAUMU IPI INAKUBALIKA MBELE ZA MUNGU?