JE NI SAUMU IPI INAKUBALIKA MBELE ZA MUNGU?

JE UMESHAWAHI KUJIULIZA NI KWA NINI TUNAFUNGA NA KUOMBA? NA JE NI SAUMU IPI INAYOKUBALIKA MBELE ZA MUNGU? WATU WENGI TUMEKUWA TUKIFUNGA NA KUOMBA LAKINI HATUPATI MAJIBU YA MAOMBI YETU KAMA WALIVYOKUWA WANA WA ISRAELI KATIKA KITABU CHA ISAYA 58:3-5 LAKINI UKISOMA KATIKA ISAYA 58:6-7 INAELEZA MAMBO 8 YA KUZINGATIA ILI SAUMU YETU IKUBALIKE MBELE ZA MUNGU NAYO NI 1. KUFUNGUA VIFUNGO VYA UOVU 2. KUZILEGEZA KAMBA ZA NIRA. 3. KUWAACHIA HURU WALIONEA 4. KUVUNJA KILA NIRA. 5. KUWAGAWIA WENYE NJAA CHAKULA CHAKO. 6. KUWALETA MASKINI WALIOTUPWA NJE NYUMBANI KWAKO. 7. UMWONAPO MTU ALIYE UCHI, UMVIKE NGUO 8. WALA USIJIFICHE NA MTU MWENYE DAMU MOJA NAWE. BASI NDUGU TUZINGATIE MAMBO HAYA ILI MAOMBI NA SAUMU ZETU IKUBALIKE MBELE ZA BWANA. Wako katika ujenzi wa Taifa Mwalimu Caleb Samuel Bandora. BONYEZA MAANDISHI HAYA ILI UJIUNGE NAMI NIWE NAKUTUMIA MAKALA NZURI NA MASOMO YA NENO LA MUNGU , UJASIRIAMALI, BIASHARA NA MAFANIKIO KWA NJIA YA E...