Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2017

JE KAMA UKIUTAFUTA KWANZA UFALME WA MUNGU UTAPATA NINI?

Picha
Hello habari ndugu? Karibu tena siku ya Leo tena tunapoendelea kujifunza zaidi kuhusu neno la Mungu pamoja na mbinu mbalimbali za mafanikio, ujasiriamali na biashara. Leo nitazungumzia suala la maisha yetu ya kawaida kabisa. Watu wengi tumekuwa tukihangaikia maisha ambalo ni jambo zuri sana kwa sababu ndipo tunapopapata ridhiki yetu ya kila Siku. Lakini leo ndugu nataka turudi kwenye maandiko matakatifu yaani biblia kuhusu suala la utafutaji na je inatuhasa tutafute kitu gani kwanza ili tuweze kupata mafanikio Yetu ya kimwili Na kiroho pia. Naomba usome na mimi kwenye biblia katika kitabu cha MATHAYO 6:33-34 kama ifuatavyo; 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Kwa hiyo rafiki yangu nakushauri sana jitahidi kutafuta ufalme wa Mungu kwanza kabla ya kitu chochote hapa duniani na hapo ndipo Mungu atakubariki hata kazi ya mikono yako. Una...

MADHARA UTAKAYOPATA KAMA USIPOTUMIA KIPAJI CHAKO

Picha
Leo napenda nizungumze na wewe rafiki yangu juu ya talanta au kipaji chako ulichopewa na Mungu . Yawezekana rafiki yangu wewe una kipaji cha uimbaji au uchoraji  au uandishi au uigizaji  n.k.  Pia labda wewe umepewa kipaji au Huduma Fulani ambayo unatakiwa kumtumikia Mungu kupitia hicho kipaji au Huduma uliyopewa Mungu. Lakini yawezekana haujatumia kipaji au talanta kutokana sababu au visingizio mbali mbali kama kutokujiamini , kujisikia , maringo, ulegevu, uvivu au unataka hadi ubembelezwe na sababu zingine kadhalika Naomba usome biblia  na mimi katika kitabu cha MATHAYO 25: 14-30. Hii imelezea watumishi watatu walioachiwa talanta na bwana wao. Mmoja alipewa talanta kumi, mwingine  talanta tano na mwingine talanta moja. Aliyepewa talanta kumi alienda akafanya biashara akapata talanta kumi nyingine vivyo hivyo aliyepewa talanta tano akazalisha talanta tano zingine baada ya kufanya biashara. Lakini aliyepewa talanta moja akachimba shimo akaifukia talanta yake ...